1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yazidi kushinikzwa kuhusu mpango wake wa nyuklia

18 Novemba 2011

Iran inazidi kushinikizwa kuhusu mpango wake wa nyuklia. Mkurugenzi Muu wa IAEA ameitaka Iran ijieleza kuhusu tuhuma za kuwepo mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri.

https://p.dw.com/p/Rx78
Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Yukiya AmanoPicha: AP

Serikali ya Iran ikizidi kutuhumiwa kuwa imetengeneza bomu la nyuklia kwa siri, Mkurugenzi mkuu wa IAEA, Yukiya Amano amesema, ni wajibu wake "kuutahadharisha ulimwengu" juu ya tuhuma hizo. Kwa hivyo, anaamini wakati umewadia kwa Iran kutoa majibu ya masuala mengi kuhusiana na mpango wake wa nyuklia. Amesema:

"Natoa mwito kwa Iran kushirikiana vizuri na maafisa wa IAEA bila ya kuchelewa na itoe maelezo yanayohitajiwa, juu ya uwezekano wa kuwepo uhusiano wowote wa kijeshi katika mpango wake wa nyuklia."

IAEA inataka kuipeleka tume ya wataalamu wake nchini Iran upesi iwezekanavyo, lakini hakuna tarehe maalum iliyopangwa. Hata hivyo, Amano anaamini kuwa wakati wa kuwapeleka wataalamu hao umewadia.

Je, kwa nini wakuu wa IAEA wameitoa ripoti yao yenye maelezo dhahiri kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wakati huu. Je, Amano alishinikizwa kisiasa, kama viongozi wa Iran wanavyodai? Rais wa bunge la Iran alikwenda umbali wa kusema kwamba IAEA ni chombo cha Marekani.

Mkurugenzi mkuu Amano, akiyajibu masuala hayo, amekubali kuwa ripoti yenye maelezo kama hayo haijawahi kutolewa. Sababu ni kwamba hawakujua mengi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Lakini katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wamepata habari zaidi kuhusu mpango huo. Kwa hivyo ni dhahiri kuwa kuna masuala yanayohitaji kujibiwa na Iran.

FILE- Outside view of the UN building with the International Atomic Energy Agency, IAEA, office inside, in Vienna, Austria, in this file photo dated Oct. 7, 2005. A United Nations report released Tuesday Nov. 9, 2011, suggests that Iran could be on the brink of having the capability to develop an atomic weapon, although Tehran insists that its nuclear program is for peaceful purposes, not weapons production. (Foto:Ronald Zak, file/AP/dapd)
Jengo lenye makao makuu ya IAEA mjini Vienna, AustriaPicha: dapd

Hata mataifa makuu hapo jana, yaliweka kando tofauti zao na yalikubaliana kuishinikiza Iran kutoa maelezo juu ya wasiwasi uliopo kuhusu nia ya mpango huo wa nyuklia. Mataifa hayo makuu ni Marekani, Urusi, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, zinazotafuta suluhisho la kidplomasia. Baada ya kuwa na majadiliano makali, mataifa hayo yametayarisha azimio la pamoja litakalowasilishwa mbele ya bodi ya IAEA leo hii mjini Vienna, Austria. Azimio hilo litajadiliwa na bodi hiyo yenye nchi wanachama 35 kabla ya kupigiwa kura.

Mwandishi: Paas,Jörg/ZPR

Tafsiri: Martin,Prema

Mhariri: Mohammed Khelef