1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yasema vikwazo vipya si halali

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGNA

TEHERAN:

Iran imesema,vikwazo vipya vilivyopendekezwa kuwekwa dhidi ya nchi hiyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa si halali.Siku ya Ijumaa baraza hilo lilikamilisha mswada wa azimio linalotoa mwito wa kuiwekea Iran vikwazo vipya baada ya nchi hiyo kukataa kusitisha shughuli za kurutubisha madini ya uranium. Mswada huo unatazamiwa kupigiwa kura na Baraza la Usalama siku ya Jumatatu.

Nchi za Magharibi zina wasiwasi kuwa Iran itatumia ujuzi wake wa kurutubisha uranium kutengeneza silaha za nyuklia kwa siri.Iran lakini inasisitiza kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA imesema,haiwezi kuthibitishwa iwapo mradi wa nyuklia wa Iran ni kwa matumizi ya amani.Kufuatia ripoti hiyo,Marekani na washirika wake wa Ulaya katika Umoja wa Mataifa zimehimiza kuiwekea Iran vikwazo vipya.