1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Sikiliza sauti 09:45

Waandamanaji wapambana na polisi DRC

Maelfu ya wapinzani wa Rais Jospeh Kabila wa DRC waliandamana mjini Kinshasa kumpinga kiongozi huyo. Katika Kinagaubaga Josephat Charo anazungumza na Kudura Kasongo, mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FIS, anayechambua hali ilivyo.  

Marekani na Afrika kuimarisha ushirikiano wa biashara

USA US- Africa Business Forum in New York

Rais wa Marekani Barack Obama amesifu hatua zilizopigwa katika kukuza biashara kati ya Marekani na mataifa ya Afrika. Obama ameyasema hayo wakati wa mkutano wa pili wa kilele wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika, uliofanyika mjini New York. 

Nigeria,Yola Malkohi Flüchtlingscamp

Boko Haram yasababisha janga la njaa Nigeria

Mgogoro unaosababishwa na ghasia za kundi la itikadi kali za kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria unaendelea kusababisha athari kubwa ya ukosefu wa chakula nchini humo. Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu tatizo hilo ambapo watoto 250,000 walioko chini ya umri wa miaka 5 wanatajwa kwamba huenda wakakabiliwa na utapiamlo. 

Touristen im Massai Mara National Park in Kenia

Sekta ya utalii Kenya yaimarika

Mkurugenzi wa chama cha wenye kumiliki hoteli Kenya, kanda ya Pwani, Sam Ikwaye, anazungumza na Eric Ponda katika Kinagaubaga kuelezea namna ambavyo watalii sasa wanarejea Kenya baada ya vitisho vya ugaidi kuwatia wasiwasi baadhi yao. Hoteli sasa zinaanza tena kupata wateja wakutosha. 

Sikiliza sauti 39:00

Afrika Mashariki na uhuru wa vyombo vya habari

Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na utendaji kazi wa vyombo vya habari duniani, Freedom House, inayaweka mataifa ya Afrika Mashariki katika kigawe kinachoanzia kwenye yale yasiyo kabisa na uhuru wa habari hadi yale yenye aina fulani ya uhuru wa habari. Je, hii ina maana gani katika uhalisia wa waandishi wa habari, wale hasa ambao wanaishi na kuziishi habari zenyewe?