1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliouwawa yaongezeka nchini Syria

Sekione Kitojo20 Desemba 2011

Kundi la waangalizi wa mataifa ya Kiarabu wanatarajiwa kwenda huko Syria kuangalia juu ya nchi hiyo inavyotekeleza itifaki ya makubaliano ya amani na umoja huo.

https://p.dw.com/p/13VwC
This image from amateur video made available by the Ugarit News group on Monday, Dec. 12, 2011, purports to show security forces in Daraa, Syria. (Foto:Ugarit News Group via APTN/AP/dapd) THE ASSOCIATED PRESS CANNOT INDEPENDENTLY VERIFY THE CONTENT, DATE, LOCATION OR AUTHENTICITY OF THIS MATERIAL. TV OUT
Syrien / Daraa / SicherheitskräftePicha: dapd

Wanaharakati wa haki za binadamu , wamesema zaidi ya watu 100 wameuwawa nchini Syria , wakati umoja wa nchi za Kiarabu , Arab League , umetangaza kuwa utapeleka nchini humo , ujumbe maalum wa mwanzo wiki hii, kusafisha njia kwa ajili ya kupelekwa kundi la waangalizi ambao watajaribu kusaidia kumaliza ghasia zilizodumu miezi tisa sasa nchini Syria.

Kundi linalochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria limesema jana kuwa zaidi ya wanajeshi 60 waliolikimbia jeshi la serikali wamepigwa risasi na kuuwawa na jeshi la serikali wakati wakijaribu kukimbia kutoka katika kambi yao, hiyo ni kwa mujibu wa maelezo ya wale walionusurika ambao wamejeruhiwa. Kundi hilo pia limetoa hesabiu ya raia 40 ambao wameuwawa kwa risasi nchini Syria katika ukandamizaji wa waandamanaji.

Kundi hilo linalofanya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake mjini London limesema kuwa wanajeshi watatu wameuwawa katika mapigano na waasi waliokimbia jeshi wanaounga mkono upinzani katika jimbo la Idlib. Shirika la habari la serikali SANA limesema kuwa majeshi ya usalama yameuwa mtu mmoja ambaye ametajwa kuwa ni gaidi na kuwajeruhi wengine kadha.

Mauaji hayo yametokea siku hiyo hiyo ambapo Syria imekubali kuruhusu mataifa ya Kiarabu kuchunguza utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya nchi hiyo na umoja wa mataifa ya Kiarabu , yenye lengo la kuzuwia ghasia dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali.

Umoja wa mataifa umesema kuwa zaidi ya watu 5,000 wameuwawa tangu maandamano yaanze. Syria imesema kuwa zaidi ya wanajeshi 1,100 wameuwawa na kundi la kigaidi linaloungwa mkono na mataifa ya kigeni.

Umoja wa mataifa ya Kiarabu, Arab League , ambao umeiwekea vikwazo vya kiuchumi Syria, umetishia kulipeleka suala hilo katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle hata hivyo anasisitiza zaidi kuhusu kupatikana azimio la umoja wa mataifa kuhusu Syria.

Berlin/ Aussenminister Guido Westerwelle (FDP) kommt am Mittwoch (14.12.11) in den Plenarsaal im Bundestag in Berlin. Foto: Maja Hitij/dapd
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido WesterwellePicha: dapd

Mtazamo wangu ni kwamba ni suala la muda tu , ambapo mataifa yanayowakilishwa katika baraza la usalama la umoja wa mataifa yatabadili msimamo wao. Ni lazima tutoe jibu la wazi pamoja na mbinyo kuhusiana unyama unaotokea nchini Syria

Hata hivyo mkuu wa umoja wa mataifa ya kiarabu amesema baada ya kutiwa saini kwa itifaki ya kuruhusu wachunguzi wa kigeni kuwa hakuna mpango wa kuondoa vikwazo ambavyo vimewekwa wakati Syria ilipokataa wachunguzi wa kigeni. Nabil Elraby amesema kuwa wachunguzi hao sasa itakuwa ni sababu ya kuamua iwapo serikali ya Syria inatekeleza makubaliano. Katika ishara nyingine ya mbinyo wa kimataifa , baraza kuu la umoja wa mataifa limepiga kura kushutumu matumizi ya nguvu ya Syria kuzima maandamano nchini humo, ambapo Urusi na China hazikupiga kura.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri : Abdul-Rahman, Mohammed