1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliouwawa Syria yafikia watu 90

Mohamed Dahman26 Mei 2012

Baraza la Kitaifa la upinzani nchini Syria limeutaka Umoja wa Mataifa kuitisha kikao cha dharura kujadili mauaji ya takriban watu 90 yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya serikali katika mji wa Houla Ijumaa (25.06.2012).

https://p.dw.com/p/152w4
A Syrian rebel runs for cover at the Sunni district of Jabb al-Jandali in Homs, Syria, Monday, May 14, 2012. Syrian troops shelled the rebel-held town, sparking intense clashes that sent bloodied victims flooding into hospitals and clinics, activists said. The violence around the country is eroding an internationally brokered peace plan that many observers see as the last hope to calm the 14-month-old crisis. Arabic writing on the wall is an advertisement. (Foto:Fadi Zaidan/AP/dapd)
Mwanajeshi wa Syria mjini HomsPicha: AP

Kituo cha Uangalizi wa Haki za Binaadamu nchini Syria kimezishutumu jumuiya za Kiarabu na Kimataifa kwa kutowa ushirikiano wao kwa mauaji hayo yalioanza Ijumaa na kuendelea usiku kucha. Nalo Jeshi Huru la Syria kwa mara nyengine tena limetowa wito kwa mataifa makubwa kufanya mashambulzi ya anga dhidi ya vikosi vya Rais Bashar al Assad.

Mauaji hayo yanakuja wakati Kofi Annan mjumbe wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Waarabu kwa Syria ambaye alisimamia makubaliano ya kusitisha mapigano mwezi uliopita yaliokiukwa mara kadhaa,akikamilisha mipango ya kurudi tena Damascus.

Kituo hicho cha Haki za Binaadamu chenye makao yake mjini London Uingereza kimesema kwamba mashambulizi hayo ya mizinga yameuwa zaidi ya watu 90 wakiwemo watoto 25 huko Houla.Shirika hilo limeishutumu jumuiya ya kimataifa kwa kukaa kimya wakati utawala wa Syria ukifanya mauaji hayo.

U.N.-Arab League envoy Kofi Annan reads a statement after his meeting with Syria's President Bashar al-Assad in Damascus March 11, 2012. Annan said he was optimistic after a second round of talks with Assad on Sunday, but acknowledged it would be difficult to reach a deal to halt the bloodshed. REUTERS/Khaled al-Hariri (SYRIA - Tags: CIVIL UNREST POLITICS) // Eingestellt von wa
Mpatanishi wa Mgogoro wa Syria Kofi AnnanPicha: Reuters

Mikanda ya video iliowekwa kwenye mtandao wa You Tube imeonyesha taswira ya kutisha ya maiti za watoto zilizolala sakafuni baadhi ya maiti hizo zikiwa zimepasuka vibaya na sehemu ya kichwa cha mtoto mmoja kikiwa kimeripuliwa.

Awali msemaji wa kike wa Baraza la Kitaifa la upinzani wa Syria Basma Kodmani alisema zaidi ya watu 110 waliuwawa na vikosi vya serikali ya Syria na nusu yao wakiwa ni watoto. Amesema baadhi ya wahanga waliripuliwa na mizinga na kuna baadhi ya familia nzima zilizoangamizwa.

Timu ya waangalizi wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa walioko nchini Syria wamekwenda katika mji wa Houla kutathmini hali hiyo.Timu hiyo imewasili katika kijiji cha Taldau kilioko ukingoni mwa mji wa Houla kushuhudia uhalifu uliotendeka katika kipindi cha saa 24 ukiwa ni ukiukaji wa usitishaji wa mapigano.

Repoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon imesema makundi yanayompinga Assad yanadhibiti sehemu kubwa za baadhi ya miji na kwamba kuna uharibifu mkubwa sana nchini kote.

epa03088377 UN Secretary-General Ban Ki-moon speaks during a joint press conference with the Palestinian Authorities President Mahmoud Abbas (unseen) in the West Bank town of Ramallah on 01 February 2012. UN Secretary-General Ban Ki-Moon kicked off a series of meetings 01 February with Israeli and Palestinian leaders, holding talks in Jerusalem with President Shimon Peres. EPA/ATEF SAFADI
Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moonPicha: picture-alliance/dpa

Repoti hiyo inayotarajiwa kujadiliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki ijayo inasema kuna mzozo unaoendelea nchini Syria ukiandamana na umwagaji damu wa kila siku,kuzidi kuwa mbaya kwa hali ya kibinaadamu, ukiukaji wa haki za binaadamu na kuendelea kwa malumbano ya kisiasa.

Annan alisimamia kufikiwa kwa makubaliano ya mpango wa amani wa vipengele sita wenye kujumuisha usitishaji wa mapigano ulioanza kufanya kazi tarehe 12 mwezi wa April na ambao umekuwa ukikiukwa kila siku.

Ahmad Fawzi msemaji wa Annan amesema mjumbe huyo anatazamiwa kwenda Syria hivi karibuni kuendeleza juhudi za kutafuta ufumbuzi wa amani kwa mzozo huo. Wanadiplomasia huko Geneva wamesema katibu mkuu huyo wa zamani wa Umoja wa Mataifa atakwenda Damascus mapema wiki ijayo.

Kufuatia shambulio hilo la Houla Jeshi Huru la Syria limetowa wito kwa kundi la mataifa Marafiki wa Syria kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vya serikali ya nchi hiyo. Generali Mustafa Ahmed al- Sheikh anayeongoza baraza la kijeshi la Jeshi Huru la Syria alieko Uturuki ametowa wito wa kuchukuliwa kwa hatua inayofaa kufuatia mauaji hayo ya kinyama huko Houla.

Ametaka kuanzishwe kwa muungano wa kijeshi nje ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza mashambulizi maalum ya anga dhidi ya magenge ya Assad na taasisi zake kuu.

Marekani,Ufaransa,Uingereza, Ujerumani na mataifa ya Kiarabu ya Saudi Arabia na Qatar yanaongoza katika kundi la Marafiki wa Syria wenye kutaka kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya utawala wa Assad.

Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP
Mhariri: Sudi Mnette