1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa katika ghasia za Kenya ni zaidi ya 300

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClQ8

NAIROBI:

Watu wengine saba wameuawa katika ghasia mpya nchini kenya.

Mauaji hayo yametokea katika wilaya ya Trans-Nzoia magharibi mwa Kenya walipojaribu kukishambulia kituo cha Polisi ambako watu walioachwa bila makazi na ghasia hizo walikokuwa wamepiga kambi.

Kwa mda huohuo juhudi za kuwasaidia watu laki 2 walioachwa bila makazi naghasia za kikabila zinaendelea.Shirika la mpango wa chakula dunianiWFP umetuma magari 20 yenye chakula kutoka Mombasa hadi Nairobi.

Na habari zingine zinasema Rais Levy Mwanawasa wa Zambia ameomba kufanyika kwa mjadala halisi nchini Kenya kufutaia ghasia za kisiasa ambapo wasiopungua 300 waliuliwa.

Katika taarifa iliotolea mjini Lusaka,rais Mwanawasa ,ambae ni mwenyekiti wa jumuia ya ushirikiano wa maendeleo kusini mwa Afrika-SADC-,amemhimiza cheo somo wake wa Kenya- Mwai Kibaki pamoja na kiongozi wa upinzani Kenya Riala Odinga kuzungumza kwa ajili ya kupatikana amani.

Amsema kuwa Kenya imekuwa kitovu cha amani katika kanda ya Afrika Mashariki na imetoia mchango mkubwa ya kuleta amani nchini Somalia na maeneo mengine yenye migogoro barani Afrika.Idadi ya walifariki kutokna na ghasia za bada ya uchaguzi nchini Kenya,kwa mujibu wa shirika la habari la AFP imefikia 371.