1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi kubwa ya watu wameuawa Afghanistan

19 Aprili 2016

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema watu wengi waliuawa katika mji mkuu ,Kabul lakini bila ya kutaja idadi kamili. Taarifa zinasema wapiganaji wa Taliban wameshambulia makao makuu ya idara ya upelelezi

https://p.dw.com/p/1IYBY
Afghanistan Explosion in Kabul
Eneo lililotokea mripuko mjini KabulPicha: Reuters/O. Sobhani

Mji wa Kabul kwa mara nyingine ulikumbwa na mashambulio mapema leo asubuhi. Mpaka sasa idadi kamili ya watu waliouliwa haijajulikana kutokana na mashambulio hayo lakini taarifa zinasema maafisa wasiopungua 15 wa idara ya ujasusi walikuwa miongoni mwa waliouawa.

Afisa mmoja wa idara ya usalama wa taifa ambae hakutaka kutajwa jina , aliitoa taarifa hiyo.

Mtu mwengine ambae ni mshauri na msemaji wa masuala ya afya kwenye wizara ya afya Ismail Kawusi amefahamisha kuwa watu wasiopungua 200 walijeruhiwa katokana na shambulio hilo

Wanajeshi wamejeruhiwa

Kwa mujibu wa msemaji wa hospitali ya majeruhi ya mji wa Kabul,wanajeshi na raia pia walikuwa miongoni mwa majeruhi. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan Sediq Sediqi ameeleza kuwa idadi ya watu waliokufa ni kubwa zaidi kwa sababu shambulio hilo la kujitoa mhanga lilifanywa wakati ambapo panakuwepo misongamano mikubwa ya watu katika mji wa Kabul.

Afghanistan Explosion in Kabul
Sehemu ya athari za mripukoPicha: picture-alliance/dpa/J. Jalali

Wakati nilipokuwa nafanya kazi nilisikia mripuko mkubwa.Sehemu yote ilifunikwa na vumbi.Kwanza sikuweza kuona kilichokuwa kinatokea.Lakini baadae niliweza kubainisha kwamba madhara makubwa yalitokea.

Msemaji wa Taliban Mujahid amedai kwamba kundi hilo la lilihusika na shambulio hilo. Wapiganaji wa kundi hilo wameimarisha hujuma zao dhidi ya majeshi ya usalama tangu watangaze, wiki iliyopita, kampeni mpya ya mashambulizi ya msimu wa mabubujiko .

Shambulio hilo ni la kwanza katika mji wa Kabul kufanywa na Taliban tangu watangaze mpango wao.

Taliban pia wamefanya mashambulio katika majimbo mengine Afghanistan tangu wautangaze mpango wao wa mashambulizi.

Rais wa Afghan Ashraf Ghani ameyalaani vikali mauaji yaliyofanywa leo asubuhi kwenye kitongoji cha Puli Mahmood Khan katika mji mkuu , Kabul. Rais Ghan amewalaani , aliowaita magaidi waliofanya mauaji.

Amesema mashambulio hayo hayataivunja ari na dhamira ya majeshi ya usalama ya kupambana na magaidi hao.

Msemamji wa Taliban amedai kwamba wapiganaji wao waliweza kuingia ndani ya ofisi za idara ya usalama wa taifa .

Maafisa wa serikali hawakuthibitisha madai hayo lakini habari zinasema milio ya risasi ilisikika. Kuibuka tena kwa wapiganaji wa Taliban kunazua maswali mengi juu ya uwezo wa majeshi ya serikali ya Afghanistan.

Mwaka uliopita askari 5500 waliuliwa.

Mwandishi:mtullya abdu./afpe/rtre.
Mhariri: Iddi Ssessanga