1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hong Kong. Kumbukumbu ya kuikabidhi Hong Kong kwa China.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmx

Rais wa China Hu Jintao amehutubia leo katika tukio la kuadhimisha mwaka wa kumi tangu koloni hilo la zamani la Uingereza kurejeshwa kwa China mwaka 1997.

Rais Hu ameahidi kuimarisha utawala bora wa wananchi katika jibu la miito kadha ya wananchi wa Hong Kong wakitaka uchaguzi wa moja kwa moja ifikapo mwaka 2012.

Rais Hu ameahidi kuimarisha demokrasia zaidi na kusema kuwa demokrasia katika Hong Kong inakua katika njia iliyo sahihi.

Kwa hivi sasa jimbo hilo linatawaliwa na baraza ambalo linateuliwa na watu wanaopendelea serikali ya China mjini Beijing , ikiwa nusu ya wabunge wake 60 ndio wamechaguliwa moja kwa moja na wananchi.