1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HECHICERA:Utoaji mimba wahalalishwa

25 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7J

Wajumbe katika jiji la Mexico wamepiga kura kuunga mkono mswaada wa kuufanya utoaji mimba kuwa sheria na hatua hiyo inatarajiwa kuchochea maamuuzi kama hayo katika sehemu zingine za Latin Amerika.

Mswaada huo ulipitishwa kwa kura 46 dhidi ya kura 19 utaanza kutekelezwa mara tu meya wa jiji la Mexico atakapotia saini na kuuidhinisha kuwa sheria.

Azimio hilo limeleta mgawanyiko katika nchi ambayo inafuata zaidi maadili ya dini ya kikiristo ya kanisa katoliki.

Iwapo meya wa jiji la Mexico atatia saini mswaada huo basi jiji hilo litakuwa la pili katika eneo hilo baada ya mswaada kama huo kupitishwa nchini Cuba.

Wanaharakati wanaopinga kuhalalishwa utoaji mimba wanajadili hatua watakazochukua baada ya mswaada huo kupitishwa na wajumbe.