Havana. Castro hakuhudhuria kikao cha mwishoni mwa mwaka. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Havana. Castro hakuhudhuria kikao cha mwishoni mwa mwaka.

Kiongozi wa Cuba Fidel Castro ambaye anaugua amekosa kuonekana katika kikao cha mwisho cha mwaka cha bunge la nchi hiyo, ikiwa ni ishara kuwa utawala wake wa karibu nusu karne unakaribia kwisha.

Kiti ambacho kwa kawaida hukaliwa na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 katika kituo cha mikutano mjini Havana kilikuwa tupu katika mkutano huo, ambao uliongozwa na mdogo wake wa kiume Raul Castro na wajumbe wengine wa uongozi wa chama cha kikomunist katika kisiwa hicho.

Castro hajaonekana hadharani tangu mwezi Julai mwaka

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com