HAVANA : Castro ashindwa kuhudhuria gwaride | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAVANA : Castro ashindwa kuhudhuria gwaride

Fidel Castro ameshindwa kuhudhuria ufunguzi wa gwaride la kijeshi kwa heshima yake leo hii huku kukiwa na hali ya mashaka juu ya afya ya kiongozi huyo wa Cuba alie mgonjwa.

Kaimu kiongozi wa Cuba Raul Castro ambaye ni mkuu wa ulinzi wa nchi hiyo alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo.

Matarajio makubwa ya Wacuba ambayo ingawa yaliandamana na mashaka yalilenga juu ya iwapo au la Fidel Castro atajitokeza kwenye gwaride hilo la kijeshi ambalo linafanyika nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Kujitokeza kwa kiongozi huyo kwa njia yoyote ile hata kwenye kioo cha televisheni kungeliweza kutowa mwanga iwapo kamanda huyo aliyeiongoza Cuba kwa zaidi ya miongo minne ataweza kamwe kushika tena hatamu ya kuiongoza nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com