Hatima ya Samuel Eto′o kukatwa leo. | Michezo | DW | 14.02.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Hatima ya Samuel Eto'o kukatwa leo.

Hatima ya stadi wa Kamerun katika FC barcelona inazingatiwa leo huku timu kadhaa za Ulaya zikijiwinda kwa changamoto 32 za kesho za Kombe la UEFA.Brazil haiko tena killeleni mwa timu bora za dunia.

Mabingwa wa dunia wa dimba Itali, wameipopoa kutoka kileleni Brazil kama timu bora ya dunia.FC Barcelona inazingatia hatima ya samba wa nyika Samuel Eto’o iwapo imsimamishe kucheza au la.

Kombe la shirikisho la dimba la Ulaya-UEFA linarudi uwanjani kesho huku bayer Leverkusen ya Ujerumani ikiwa na miadi na Blackburn Rovers ya Uingereza .

Kombe la Ulaya la UEFA linarudi kesho uwanjani kwa mapambano yake 32 ya mwisho.Bayer Leverkusen ya Ujeruma ni inakutana kesho na Blackburn Rovers ya Uingereza na kocha wa Blackburn Mark Hughes ameshampa changamoto muafrika Kusini Beni McCarthy kuionesha Leverkusen kilichomtoa kanga manyoya.McCarthy ameshashinda kombe la klabu bingwa la Ulaya wakati akiichezea FC porto ya Ureno na sasa atazamiwa kutamba pia katika kombe hili la UEFA.

Stadi mwengine wa Afrika anaepewa changamoto ni mkamerun Samuel Eto’o ambae hatima yxake huenda ikajulikana leo katika klabu ya FC Barcelona.Eto’o alieumia muda mrefu na ndio kwanza amerudi uwanjani,amemshambulia kocha Frank Rijkaard kwa kumtuhumu eti hapendi kuichezea Barcelona na Ronaldinho nae akamtuhumu Eto’0 haoneshi ari ya kucheza na wenzake.Tuhuma hizo zikamkasirisha Samuel Eto’o na akafoka.

Eto’o aliudhika kumsikia kocha katika ukumbi na waandishi habari na kusema hakutaka kucheza.Alisema kudai hivyo sikusema ukweli.Kikao maalumu anafanyiwa leo Eto’o kujua atasamehewa au ataadhibiwa.

Brazil haiku tena kileleni mwa ngazi ya FIFA kama ndio timu bora duniani wakati huu.Mabingwa wa dunia Itali licha ya machafuko ya wahuni katika Ligi za nyumbani imeipiku Brazil na kuparamia binafsi kileleni mwa ngazi ya FIFA.Itali mara ya mwisho kuwa kileleni ilikua 1993.Timu 6 chini ya Itali na Brazil hazikubadilika nafasi zao-Argentina,Ufaransa,Ujerumani,Uingereza,Holland na Ureno.

Mexico inapanga kugombea kuandaa Copa Amerika-kombe la mataifa ya Amerika kusini mwaka ujao –mwaka mmoja kabla kuchezwa kmombe lijalo 2009.

Kwa upande mwengine, India,Iran na Qatar zinaania kuandaa Kombe la Asia la mataifa kwa mwaka 2011.uamuzi wapi kombe litachezwa mwaka huo utakatwa Julai 28, siku moja kabla ya finali ya Kombe la Asia la mwaka huu.

Katika vita vya kupambana na madhambi ya Doping,Dick Pound,mkuu wa shirika la dunia linalopiga vita doping (WADA) alisema leo kwamba kukaripiwa na halmashauri kuu ya olimpik ulimwenguni (IOC) hakutamfunga mdomo asiulize majibu ya maswali yanayohusiana na tuhuma kuwa bingwa mara kadhaa wa mbio za baiskeli za wa tour de France-muamerika Lance Armstrong alitumia madawa kutunisha misuli. Dick pound alinukuliwa kusema,

“Ikiwa Armstrong anadhani hii itanifanya nitoweke basi amekosea.”

Wachezaji wa cricket wa Kenya kwa kushinda mashindano ya dunia ya Ligi kila mmoja atachota kitita cha dala 5,000.

 • Tarehe 14.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcf
 • Tarehe 14.02.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcf