Hatima ya Mazungumzo ya Amani Mashariki ya Kati baada ya Aprili 29
29 Aprili 2014Baada ya kushindikana kwa juhudi thabiti za kidiplomasia zilizochukua muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwa lengo la kuleta suluhisho la mgogoro wa mashariki ya kati hadi kufikia leo ,subira ya mpatanishi-Marekani imezidi kupungua kutokana na Israel na Wapalestina kujiweka kando ya juhudi za mazungumzo.
Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry bado ameeleza matumaini kwa kusisitiza kwamba mchakato wa mazungumzo ya kuleta amani katika mashariki ya kati bado haujazimika. Hata hivyo Waziri Kerry ameeleza kuwa mchakato huo umeingia katika hatua ya makabiliano , katika upande mmoja na mkwamo katika mwingine.
Lakini pande zote kuu za mchakato wa masharriki ya kati, Israel na Wapalestina zimeshafanya maamuuzi yao .
Kufuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili za Wapalestina,Hamas na Fatah ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa,Israel imeamua kuyavunja mazungumzo.
Israel haina njia nyengine,lakini suluhisho la muda linahitajika
Mtafiti kwenye taasisi ya masuala ya usalama ya mjini Telaviv Mark Heller amesema uamuzi wa Israel wa kuyavunja mazungumzo na Wapalestina unaweza kueleweka.Mark Hall ameeleza kwamba haina maana kwa Israel kufanya mazungumzo ikiwa upande mmoja hautaki.Hata hivyo mtaalamu huyo ameshauri kwamba madhali mazungumzo yamesimama, inapasa kutafuta suluhisho la muda.Ameeleza.Watu wengi wana maoni kwamba, pamoja na kufanya juhudi za kuuendeleza mchakato wa mazungumzo ya kuleta amani, hatua nyingine zinaweza kuchukuliwa, kama suluhisho la mpito.
Kwa mfano ingefaa kuyahamishia kwa mamlaka ya Wapalestina madaraka ya utawala ya sehemu za Wapalestina zinazodhibtiwa sasa na Israel."
Waziri Mkuu w a Israel Benjamin Netanyahu amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika baina ya Israel na serikali yoyote mpya ya Wapalestina mpaka hapo Hamas itakapoitambua Israel.
John Kerry akanusha tuhuma za kuilinganisha Israel na nchi ya kibaguzi
Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John kerry amekanusha vikali, kuifananisha Israel na iliyokuwa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini. Baada ya kutolewa miito mikali ya kumtaka ajiuzulu, au angalau aombe radhi, Kerry amesema haamini iwapo alisema hadharani au kwa faragha kuwa serikali ya Isreal ni ya kibaguzi kama ile ya Afrika Kusini ya hapo awali.
Lakini mjumbe mkuu wa Wapalestina kwenye mazungumzo na Israel Saeb Erakati ameilaumu Israel. Erakat amesema ikiwa amani haiwezi kufikiwa bila ya ushiriki wa Gaza, na kwa hakika haiwezi kufikiwa bila ya Ukanda wa Gaza, basi Israel inalenga shabaha nyingine, yaani ya kutofikia amani.
Lakini mbunge mmoja wa Israel, Tzahi HaNegbi aliepo karibu na Waziri Mkuu Netanyahu ameimbia radio ya jeshi kwamba Israel inapasa kusubiri na kuielewa maana ya makubaliano yaliyofikiwa baina pande mbili za Wapalestina.
Mwandishi:Mtullya abdu/afpe
Mhariri.Hamidou Oummilkheir