1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Mugabe apitishwa kugombea urais kwa mara nyingine

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDc

Kamati kuu ya chama cha ZANU PF nchini Zimbabwe imemchagua rais Robert Mugabe agombee tena wadhifa wa rais mwaka ujao.Uamuzi huo ulipitishwa kwenye mkutano wa chama hicho mjini Harare.

Chama cha upinzani ,MDC kimesema uamuzi huo ni maafa kwa Zimbabwe.

Chama hicho kimesema kuwa rais Mugabe ambae sasa ana umri wa miaka 83 ameshaivuruga Zimbambwe katika utawala wake wa miaka 27.Na msemaji wa Ikulu ya Marekani ameeleza kuwa uamuzi wa kumchagua Mugabe agombee urais kwa mara nyingine ni jambo la kusikitisha na kukasirisha.