HARARE : Wanajeshi mbaroni kwa kutaka kupinduwa | Habari za Ulimwengu | DW | 15.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE : Wanajeshi mbaroni kwa kutaka kupinduwa

Kundi la wanajeshi limetiwa mbaroni nchini Zimbabwe kwa madai ya kupanga njama za kumpinduwa Rais Robert Mugabe na nafasi yake kumuweka waziri mmoja alieko katika serikali.

Repoti ya gazeti la kila wiki la Independent imedai leo hii kwamba imepata nyaraka za mahkama zenye madai hayo.

Gazeti hilo linadai kwamba watu sita akiwemo afisa wa zamani wa jeshi na wanajeshi wengine wawili wanaotumika jeshini hivi sasa wako mbaroni baadhi yao wakiwa wametiwa nguvuni tokea mwezi wa Mei.

Kwa mujibu wa gazeti hilo watu hao wanashtakiwa kwa uhaini kwa kutaka kumpinduwa kiongozi huyo wa muda mrefu nchini Zimbabwe ambaye umashuhuri wake unaonekana kufifia na nafasi yake kumpa waziri wa Nyumba Vijijini Emmerson Mnangagwa ambaye aliwahi kuwa kipenzi cha Mugabe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com