1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Viongozi wa upinzani wafikishwa mahakamani baada ya kula mkong’oto.

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJH

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai pamoja na wanaharakati wenzake karibu 50 wamefikishwa mahakamani mjini Harare, kufuatia kukamatwa kwao katika mkutano wa sala za maombi dhidi ya serikali siku ya Jumapili.

Walipelekwa hospitali kwa matibabu, hususan majeraha makubwa pamoja na maumivu mengine ya ndani ambayo wameripoti kuwa wameyapata wakiwa mikononi mwa polisi kwa kupigwa.

Akiondoka mahakamani , Tsvangirai ameahidi kuendelea na upinzani wake dhidi ya serikali ya rais Robert Mugabe. Watu hao wanabaki chini ya ulinzi wa polisi.

Kamishna wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Louise Arbour ametaka kufanyike uchunguzi huru kuhusiana na madai ya kupigwa na polisi.