1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Serikali yauonya upinzani.

15 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIw

Serikali ya Zimbabwe imeonya kuwa upinzani utagharamika vikubwa , kwa kile inachokiita kampeni ya kuleta ghasia ili kuiondoa kutoka madarakani.

Waziri wa habari wa Zimbabwe amemshutumu kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai na wanaharakati wengine kwa kuwashambulia polisi wakati wa mkutano wao uliopigwa marufuku.

Waziri huyo pia amezishutumu serikali za mataifa ya magharibi kwa kuunga mkono chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change. Tsvangirai anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kupigwa kinyama na polisi , na wafuasi wake wanasema kuwa yeye pamoja na viongozi wengine 49 wa upinzani waliteswa wakati wakiwa katika mahabusu ya polisi.

Mkutano huo ulipangwa ili kupinga sera za rais Robert Mugabe, ambazo zimesababisha hali ya mzozo wa kiuchumi nchini Zimbabwe.