1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI: Rais Bush kuitembelea Vitennam

Rais wa Marekani, George W. Bush, yuko nchini Vietnam, kushiriki katika mkutano wa kilele wa kila mwaka wa nchi wanachama wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Ashia na Pacific, ambao utazungumzia zaidi uhusiano wa kibiashara.

Rais Bush ni rais wa pili wa Marekani kuwahi kuitembelea Vietnam tokea kumalizika vita vya Vietnam miongo mitatu iliopita. Lakini ziara yake hiyo imetatizwa na siasa zinazoendelea nyumbani Marekani ambako baraza la wawakilishi limepinga sheria ambayo ingekuwa ya kihistoria ya kurejesha uhusiano wa kibiashara na Vietnam. Kutakuwa pia na mazungumzo juu ya shughuli za kinyuklia za Korea ya kaskazini katika mkutano huo wa 21. Rais Bush alikuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Australia, John Howard kuhusu Irak. Na atakutana kwa mazungumzo pia na rais wa Uchina, Hu Jintao kando na mkutano huo wa mjini Hanoi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com