Hanoi. Kimbunga chauwa watu kadha. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hanoi. Kimbunga chauwa watu kadha.

Kimbunga Lekima kimepita katikati ya nchi ya Vietnam na kuuwa watu kadha na kuharibu mamia ya nyumba. Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa watu watano wameuwawa kabla na wakati wa kimbunga hicho jana Jumatano, lakini si vifo vyote vilivyothibitishwa. Wataalamu wa hali ya hewa wamesema kuwa kimbunga hicho kilidhoofika baada ya kupita katika jimbo la kati la Quang Binh na kuelekea nchini Laos, lakini eneo lote la kati la nchi hiyo na baadhi ya maeneo ya kaskazini yameathirika . Vietnam inakabiliwa na kiasi cha vimbunga kumi kwa mwaka , na kusababisha uharibifu wa mamilioni ya dola.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com