1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG:Mmoroko auhukumiwa miaka 15 zaidi kwa ugaidi

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcA

Mahakama ya Ujerumani imemuongezea kifungo cha miaka 15 raia wa Moroko, Mounir al Motassadeq baada ya kumkuta na hatia ya shambulizi la kigaidi Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani.

Motassadeq amekuwa mtuhumiwa wa kwanza kuhukumiwa kutokana na shambulizi hilo ambapo anatuhumiwa kuwasaidia watekaji nyara wa ndege zilizobamizwa katika kituo cha kimataifa cha biashara mjini New York, na nyingine katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon.

Mwezi Novemba mwaka jana Motassadeq alihukumiwa kifungo cha miaka saba baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya abiria na wafanyakazi 246 wa ndege hizo zilizotekwa.

Pia alipatikana na hatia ya kuwa mwanachama wa mtandao wa kikaidi