Hali ya siasa Kenya yasababisha migawanyiko zaidi? | Mada zote | DW | 12.10.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Hali ya siasa Kenya yasababisha migawanyiko zaidi?

Mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Kenya umesababisha mgawanyiko hata miongoni mwa taasisi ambazo kawaida zinatakiwa kutoegemea upande wowote, kama vile taasisi za kidini, sekta ya sheria na mashirika ya kiraia.

Sikiliza sauti 03:25

Hayo ni kwa mujibu wa baadhi ya mashirika ya kijamii nchini Kenya. Katika mazingira hayo, mwananchi wa kawaida anakosa mwongozo unaoweza kushawishi maamuzi sahihi. Daniel Gakuba amezungumza na mchambuzi wa masuala ya siasa, Maimuna Mwidau akiwa mjini Mombasa kuhusu hali hiyo. Maimuna anaanza kwa kukubaliana na hoja kwamba hata taasisi zenyewe zimechanganyikiwa hivi sasa.