Hali mjini Mombasa ni shwari baada ya ghasia za siku tatu
30 Agosti 2012Matangazo
Tangu kuuwawa kwa kiongozi huyo kumekuwa na ghasia za hapa na pale mjini Mombasa, Tayari watu 24 wamefikishwa mahakamani kufuatia ghasia hizo. Kwa sasa serikali imeunda jopo la watu 11 kuchunguza mauaji ya Sheikh Rogo na pia ghasia zilizosababisha mauaji ya watu wanne wakiwemo maafisa watatu wa polisi.
Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu wa Mombasa Eric Ponda juu ya hali halisi ya mambo kwa sasa
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Mohammed Abdul-Rahman