Hakuna njia ya mkato kupata amani Mashariki ya Kati
22 Septemba 2011Matangazo
Obama amesema, anakubali kuwa Wapalestina wana haki ya kuwa na taifa lao, lakini kwanza, wanapaswa kurejea katika majadiliano ya amani pamoja na Israel na kuachana pia na matumizi ya nguvu dhidi ya jirani wao. Nchini Marekani, Obama amekuwa akishinikizwa kuiunga mkono zaidi Israel.
Marekani imesema, itatumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kulipinga ombi la Wapalestina la kutaka uanachama kamili katika umoja huo. Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amechukua msimamo tofauti na Marekani. Yeye amesema, ujumbe wa Wapalestina katika Umoja wa Mataifa unapaswa kupandishwa hadhi kama "taifa mwaangalizi" kwa muda wa mwaka mmoja na kipindi hicho, kitumiwe kupata suluhisho la amani pamoja na Israel.