1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Haiti: Zoezi la kuwatafuta manusura lakamilika

Baada ya siku 10, tokea Haiti kutingiswa na tetemeko kubwa la ardhi, zoezi la kuwatafuta walionusurika limesimamishwa, hivi leo.

default

Zoezi la kuwaokoa watu, Haiti limesimamishwa baada ya siku 10.

Serikali ya Haiti imekamilisha zoezi la kuwatafuta na kuwaokoa watu waliokwama katika vifusi kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea nchini humo wiki iliyopita. Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uratibu wa Misaada ya Kibinaadamu, imeeleza kuwa hadi sasa watu 132 wameokolewa wakiwa hai kutoka kwenye vifusi.
Spendengala für Haiti Wyclef Jean

Wyclef Jean mwanamuziki maarufu kutoka Haiti aongoza wana muziki wengine katika tafrija ya kukusanya fedha kuwasaidia watu wa Haiti: "Hope for Haiti

Jana Ijumaa watu wawili waliokolewa wakiwa hai katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, siku 10 baada ya tetemeko hilo kutokea. Watu hao, mwanamke mwenye umri wa miaka 84 na kijana mwenye umri wa miaka 22 walikuwa wadhaifu sana, lakini sasa wanaendelea vizuri. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa na Jeshi la Marekani ambao ni watoaji wakubwa wa misaada nchini Haiti zimetiliana saini mpango wa kuendelea kutolewa misaada ya dharura. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kiasi watu 100,000 wameuawa katika tetemeko hilo la ardhi na 200,000 wamejeruhiwa na wengine milioni moja wamepoteza makaazi yao.

 • Tarehe 23.01.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricla
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/LfAa
 • Tarehe 23.01.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricla
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/LfAa

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com