Haile Gabrselassie ashindwa kuvunja rekodi yake
18 Januari 2008Matangazo
Haile Gabrselassie ameshinda mashindano ya mbio za nyika za Dubai Marathon hii leo lakini akashindwa kupata dola milioni moja kwa sekunde 30 tu.
Chipukizi huyo wa Ethiopia ameshindwa kuvunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka mara ya mwisho ya saa mbili dakika nne na sekunde 26 kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili dakika nne na sekunde 53 kwa mwendo wa kilomita 42 na mita 195.
Amekimbia pamoja na wakenya Isaac Macharia na Sammy Korir, waliochukua nafasi ya pili na ya tatu.