Hadithi za vyakula: Nzuri, mbaya na zisizopendeza
Dhana zetu kuhusu vyakula zinabadilika: Chakula kinaweza kutajwa kuwa kibaya siku moja na kusifiwa siku inayofuata kwa muda mrefu au vinginevyo. Tazama baadhi ya vile unavyotakiwa kula, usivyotatakiwa.
Sumu au kiasi?
"Kahawa inasababisha saratani" au "kahawa ni mbaya kwa mishipa yako" haya ni mambo machache ambayo watu walikuwa wakisema kuhusu kahawa. Ni mbaya kwako. Lakini watafiti wanasema kahawa ni bora kuliko sifa yake-inaweza kupunguza hatari ya wewe kupata saratani.
Mvinyo
Pombe ni mbaya kwa afya yako. Lakini mvinyo mwekundu una molekuli za miujiza za resveratrol na anthocyanis. Kunywa ama usinywe? Uchunguzi wa magonjwa ya muda mrefu unaonyesha kwa wanawake, kunywa moja kwa siku ina manufaa (mbili kwa wanaume). Kisha tena takwimu za Marekani zinaonyesha mtu asiyekunywa pombe hufariki mapema kuliko wanywaji wa wastani hadi wale sugu. Kwa hiyo pombe ni nzuri?
Siagi Vs Margarini
Miaka iliyopita tuliambiwa kuepuka kula siagi na badala yake tule margarini pekee. Siagi ya kutengeneza ina asidi kidogo ukilinganisha na ile ya kutoka kwa ng’ombe. Lakini sasa watu wanaonya kwamba Margarini ni bidhaa isiyo ya asili ikijazwa kemikali na viwanda vya vyakula.
Adui wa asili
Wakati watu walipofariki kwa ugonjwa wa moyo au kiharusi, mara nyingi walisema ni Lehemu. Kama Lehemu inazuia mishipa ya damu, madaktari walisema ilipaswa kuepukwa kwa gharama zote. Hususan vyakula hatari vilikuwa ni mayai, jibini na nyama. Lakini mwili unahitaji lehemu na hata huzalisha wenyewe. Sasa, mayai yameonekana kutokuwa na athari lakini usile kupitiliza.
Mboga mboga zilizohifadhiwa
Watu wengi huepuka kula mboga zilizohifadhiwa. Wanaamini mboga hizo zina vitamini kidogo ukilinganisha ni zile mpya. Lakini mboga zilizohifadhiwa zina virutubisho kwasababu huhifadhiwa moja kwa moja mara baada ya kuvunwa na hazikai muda mrefu katika makabati kabla ya kupelekwa kwa mteja.
Samaki na virutubisho vyake vyote
Miaka michache iliyopita , ilisemekana mafuta ya Omega-3 yalikuwa ni dawa ya kila ugonjwa. Saratani, ugonjwa wa moyo, Wataalam wa afya walitushauri kumeza vidonge vya omega-3 kila siku. Lakini sasa tunajua zaidi: Ndio, asidi hizi za mafuta ni muhimu kwa baadhi ya kazi katika mwili wetu. Lakini katika hali nyingi, ziada ya virutubisho haina manufaa kabisa.
Ziada ya kitu chochote kizuri kinaweza kuwa kibaya
Vitamini ni muhimu kwa mmeng'enyo wako, hivyo ni nini kinachoweza kuwa na afya kuliko kumeza dawa za vitamini kila siku? Vitamini C hasa ilisemekana kinga ya magonjwa yote, ikiwa ni pamoja na baridi ya kawaida. Lakini utafiti haujaweza kuthibitisha hili. Kwa kweli, virutubisho vya vitamini vinaweza hata kukudhuru. Kwa uchache, ndivyo wanasema leo ...
Kwanini unywe maji kabla ya kuhisi kiu?
Asili ni nzuri sana. Tunapohitaji maji, tunapata kiu. Lakini mtu mmoja aliwahi kusema tunapaswa kunywa kabla ya kuhisi kiu - angalau lita tatu kwa siku, au zaidi. Nadharia hii inaweza kuwa na ukweli kwamba wazee mara nyingi hupoteza hisia zao za kiu. Lakini kawaida mwili wako unapaswa kufanya kazi nzuri ya kuruhusu kujua wakati unahitaji kunywa maji.
Je maziwa yana madhara?
Maziwa yana Calcium - ni nzuri kwa mifupa yako na kuimarisha mfumo wako wa kinga. Hivyo ndivyo tulivyojifunza. Lakini utafiti wa miaka mingi wa Kiswidi unaonyesha kuwa watu wanaokunywa maziwa mengi wanaweza kufa mapema. Je, sukari ya galaktosi inachangia? Hakuna anayejua. Kwa sasa, endelea kunywa maziwa, lakini kwa kiasi.
Wasiwasi wa ngano
Tovuti nyingi zinaonya juu ya madhara yake. Wanasema "huchochea miili yetu, husababisha matumbo yetu kuvuja, na husababisha magonjwa ya kuambukiza." Madaktari wengine - na waandishi - wanasema ngano huweza hata kusababisha nywele kukatika, na mawazo ya kujiua. Pamoja na ukweli kwamba hakuna utafiti wa kuunga mkono hili, wengi wameachana na nafaka hii ambayo imewakuza baba zao.
Kwamba vyakula vya asili si dhahabu
Ikiwa chakula cha kawaida kina kemikali nyingi - kama wengine wanasema - basi vyakula vya kikaboni ndivyo tunahitaji. Ni vyakula vinavyozalishwa bila mbolea za kemikali, tunaambiwa hivyo. Lakini tafiti zinaonyesha chakula cha kikaboni hakina virutubisho vingi au kwamba ni bora kwako kuliko vyakula vya kawaida. Ni ghali tu.
Chakula bora ndio maisha yenyewe
Katika mambo yote, mtindo wa maisha ndio kitu muhimu. Takwimu zinaonyesha wazi kwamba uvutaji sigara, unywaji wa kupindukia, na uzito mkubwa ni mbaya kwa afya na vinaweza kukuua. Lakini hupaswi kuhofia sana juu ya ripoti za kuponda chakula kimoja dhidi ya kingine. Katika yote usifanye kupitiliza.