1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hadi 1,000 wameuawa katika machafuko ya Kenya

6 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D39q

NAIROBI:

Idadi ya watu waliouawa nchini Kenya katika mapambano yaliyozuka kufuatia uchaguzi wa rais nchini humo imepindukia 1,000 na 300,000 wengine wamepoteza makazi.Hayo ni kwa mujibu wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Kenya.Tume ya Umoja wa Mataifa inakwenda Kenya na itabakia huko kwa majuma matatu.Wakati huo,maafisa hao watazungumza na wajumbe wa serikali na upinzani Vile vile watawahoji mashahidi na maafisa wa mashirika yasio ya kiserikali.

Wakati huo huo pande zinazohasimiana,zimeanza kufanya majadiliano ya kumaliza umwagaji damu uliozuka nchini Kenya baada ya Rais Mwai KIbaki kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanywa Desemba 27.Kiongozi wa upinzani Raila Odinga na wafuasi wake wanasema,uchaguzi huo ulifanyiwa udanganyifu.Aliekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anaongoza majadiliano ya mjini Nairobi kati ya wajumbe wa serikali na upinzani.