Habusi 1 auwawa Texas,Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Habusi 1 auwawa Texas,Marekani

HOUSTON,TEXAS:

Nchini Marekani,mtu aliekua na bunduki amemua habusi mmoja aliemtekanyara na halafu akajiua mwenyewe katika kituo kikuu chasafari za anga za juu cha NASA,huko Houston,Texas.Polisi imearifu habusi wapili- mwanamke alikutikana yuhayi.

Mkasa huu, ulizuka jana siku ya kuomboleza kuuwawa kwa watu 32 waliofyatuliwa risasi jumatatu iliopita katika chuo kikuu cha kiufundi cha Virginia na mwanafunzi wa Korea ya kusini.

Ukoo wa mwanafunzi huyo Cho Seung-Hui umeomba radhi kwa maafa waliopata hayo.Jana pia kengele za hali ya hatari zililia katika shule huko Colorado na California

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com