1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GOMA:Waasi watwaa hifadhi ya Sokwe

4 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSf

Waasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wameitwaa hifadhi kubwa ya taifa ya Sokwe Mtu iitwayo Virunga huko mashariki mwa kongo.

Hatua hiyo imezusha wasi wasi juu ya majaaliwa ya Sokwe hao.Duniani hivi sasa kuna Sokwe mtu 700 tu na kati yao hao nusu yake wako katika hifadhi hiyo ya Virunga.

Wakati huo huo jeshi la serikali ya Kongo Kinshasa limesema limefanikiwa kuwauawa wapiganaji 28 wa General Lauret Nkunda katika mapigano ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa zaidi ya watu laki moja na elfu 70 katika eneo hilo wameyakimbia makazi yao mwaka huu kutokana na mapigano.