1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GHAZNI:Taleban wakataza wahudumu kutibu mateka walio hoi

Kundi la Taleban linakataa kuruhusu kundi la wahudumu wa afya kuwatibu mateka 21 wa Korea kusini wanaoripotiwa kuwa mahututi.Wapiganaji wa Taleban wanasema kuwa watawaachia mateka hao wawili wanaoumwa endapo seriklai itawaachi wafungwa wake wawili walioko jela nchini humo.

Wahudumu hao walijitolea kuwatibu mateka hao 21 wanaoripotiwa kuwa katika hali mbaya ya afya baada ya kuwa kizuizuini kwa zaidi ya majuma mawili.Mateka hao walikamatwa walipokuwa msafarani kuelekea mjini Kabul wakiwa kwenye barabara kuu ya Kandahar katika jimbo la Ghazni.

Kwa mujibu wa msemaji wa Taleban Yousuf Ahmadi wanawake wawili kati ya 16 wanaozuiliwa wana matatizo makubwa ya kiafya.

Mazungumzo ya kujaribu kuwaokoa mateka hao yanaonekana yamekwama baada ya serikali ya Afghanistan kukataa kutimiza madai yao ya kuachiwa kwa wafungwa wao walioko jela nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com