Ghasia zaikumba Ugiriki
30 Juni 2011Polisi wa kutuliza ghasia wametumia gesi ya kutoa machozi na ya pilipili kuwatawanya waandamanaji wenye hasira. Maduka kadhaa, migahawa na majengo mengine yaliharibiwa, katika ghasia hizo.
Wapinzani wa serikali waliokuwa wakitumia mabomu ya mkono na nondo walishambulia ofisi za wizara ya fedha ambazo ziko karibu na bunge la nchi hiyo, na kuvunja madirisha pamoja na kutaka kuchoma moto jengo.
Mpango huo wa kubana matumizi, ni muhimu kwa Ugiriki ili kuweza kupata Euro bilioni 12, ikiwa ni mkopo wa dharua kutoka Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Hata hivyo, umekuwa ukipingwa na raia wengi wa nchi hiyo.
Wakati huohuo, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ugiriki inapaswa yenyewe kwanza ithibitishe kuukubali mpango huo, wa kubana matumizi na ifanye hivyo pia kwa Ulaya.