1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Umasikini pia huchochea ajira ya watoto

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsJ

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema,umasikini katika sehemu za mashambani unasababisha ajira ya watoto katika nchi zinazoendelea.Likaongezea kuwa kote ulimwenguni,zaidi ya watoto milioni 130 wanafanya kazi za kilimo-wakiwa kati ya umri wa miaka 5 hadi 14.Shirika la FAO likiadhimisha Siku ya Kupinga Ajira ya Watoto Duniani,limetathmini kuwa asilimia 70 ya watoto wanaoajiriwa hufanya akazi katika sekta ya kilimo.Waajiri wasio na maadili na ukosefu wa shule katika maeneo ya mashambani vile vile huchangia kwa sehemu kubwa katika tatizo hilo.Shirika la FAO pamoja na Shirika la Ajira la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine,limezindua ushirikiano mpya kupambana na ajira ya watoto.