Geneva: Uchaguzi mkuu nchini Uswisi. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Geneva: Uchaguzi mkuu nchini Uswisi.

Uchaguzi mkuu unafanyika nchini Uswisi . Chama cha mrengo wa kulia Peoples Party kinatarajiwa kurudi madarakani. Chama hicho kimeendesha kampeni yenye mabishano kikitoa wito wa kurejeshwa makwao wageni wanaohusika na makosa makubwa ya uhalifu. Kampeni yake iliokosolewa vikali ni pamoja na mabango yenye picha ya nguruwe watatu weupe wakimuondoa nchini nguruwe mweusi. Wapinzani wa chama hicho wanasema hali hiyo inaweza kuhujumu sura ya Uswisi nchi za nje.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com