1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Ziara ya Condolezza Rice Mashariki ya Kati

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6J

Nchini Palestina afisa wa Hamas ameuwawa katika eneo la Ukingo wa magharibi mwa mto Jordan na watu waliojificha nyuso zao wakati akitoka msikitini kwenye kijiji cha Hebleh.

Tukio hilo limekuja siku moja baada ya chama cha Fatah cha rais Mahmoud Abbas kutishia kuwauwa viongozi wa kundi la Hamas wakati mvutano wa madaraka baina ya makundi hayo mawili hasimu ukienea nchini humo.

Ghasia kati ya makundi hayo mawili Hamas na Fatah zilizozuka wiki hiizimesababisha kuwawa kwa watu 12 na ndizo ghasia mbaya zaidi kutokea tangu mwaka 1994.

Viongozi wa nchi za kirabu pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice ambaye yuko katika ziara yake ya siku tano mashariki ya kati ,wamezitolea mwito pande zote mbili kumaliza mgogoro huo.

Rice anatarajiwa kuwa na mazungumzo baadae leo hii na rais Hosni Mubarak wa Misri juu ya kuanzisha tena mpango wa amani katika eneo hilo.

Baadae ataelekea Nchini Israel kukutana na viongozi wa nchi hiyo.