GAZA:Watoto watatu wakipalestina wauwawa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 30.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Watoto watatu wakipalestina wauwawa Gaza

Watoto watatu wakipalsetina wameuwawa na baada ya wanajeshi wa Israel kushambulia kwa kombora eneo la kaskazini mwa Gaza.

Kwa mujibu wa madaktari wa Palestina watoto wawili wakiume walio na umri wa 10-12 walikufa kutokana na kupata majeraha mabaya.Mtoto mwingine wa kike mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa amejeruhiwa vibaya kufuatia shambulio hilo alifariki kwenye hospitali.

Jeshi la Israel limethibitisha kufanya shambulio hilo na kusema kuwa lilidhamiriwa kuwalenga wanamgambo wanafyatua roketi katika ardhi yake.

Maafisa wameelezea masikitiko yao kufuatia vifo hivyo vya watoto wasio na hatia lakini wamesema i kundi la wanamgambo ndilo linalobeba dhamana ya tukio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com