GAZA.Wanajeshi wa Israel wamewauwa watu wanne
12 Oktoba 2006Matangazo
Majeshi ya Israel yamewauwa wapalestina watano akiwemo mtoto wakati yaliposhambulia Ukanda wa Gaza.
Majeshi hayo ya Israel yakipewa ulinzi na ndege za helikopta yaliingia katika kijiji cha Abassan katika operesheni ya kumsaka mwanajeshi wao aliyetekwa nyara miezi minne iliyopita.
Kwa mujibu wa jeshi la Israel Wanajeshi wake walilazimika kujibu mashambulio wakati waliposhambuliwa na wapiganaji wa Kipalestina.