GAZA:Nyumba ya mbunge yapigwa kombora katika Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 11.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Nyumba ya mbunge yapigwa kombora katika Ukanda wa Gaza

Jeshi la Israel la limeishambulia kwa roketi nyumba ya mbunge wa serikali ya chama cha Hamas kwenye Ukanda wa Gaza . Msemaji wa jeshi hilo ameeleza kuwa shambulio hilo lilielekezwa kwenye kiwanda cha silaha.

Hakuna habari iwapo madhara yametokea kwenye nyumba ya mbunge huyo Mariam Farhat

Israel imesema wakaazi wa sehemu hiyo walipewa habari mapema juu ya shambulio .

Bibi Farhat alichaguliwa kuwa mbunge baada ya chama cha Hamas kushinda katika uchaguzi wa Palestina mnamo mwezi januari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com