GAZA:Mashambulizi ya Israel yaua Wapalestina wanane | Habari za Ulimwengu | DW | 21.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Mashambulizi ya Israel yaua Wapalestina wanane

Israel imeendelea na mashambulizi yake ya makombora huko Gaza ambapo watu wanane wameuawa.

Mashuhuda wamesema kuwa makombora ya Israel yalishambulia nyumba ya mbunge wa kundi la Hamas Khalil al-Haya ambaye wakati wa shambulizi hilo hakuwepo.Kati ya waliyouawa ni ndugu sita wa mbunge huyo.

Israel imesema kuwa nyumba ya mbunge huyo haikuwa lengo la shambulizi hilo.

Mapema Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert alisema kuwa mashambulizi zaidi yataendelea ikiwa ni kulipiza kisasi kutokana na mashambulizi ya maroketi yanayofyatuliwa na kundi la Hamas dhidi ya Israel.

Hayo yakiendelea wapatanishi wa mzozo kati ya vyama hasimu huko Palestina, vya Hamas na Fatah wamesema kuwa vyama hivyo vimefikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Katika mapigano ya hivi karibuni kati ya vikundi hivyo viwili, kiasi cha wapalestina 49 wameuawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com