GAZA:Israel yafanya mashambulio ya angani gaza City
10 Juni 2007Matangazo
Israel imefanya mashambulio ya angani dhidi ya majumba yanayotumiwa na kundi la wanamgambo wakipalestina la Islamic Jihad na wanachama wa Fatah huko Gaza City.
Shambulio hilo limetokeo saa chache baada ya kufanyika uvamizi katika eneo la mpaka kati ya kituo cha wanajeshi wa Israel na mashariki mwa ukanda wa Gaza na Israel.
Wanamgambo wa Islamic Jihad wanadai kuhusika na uvamizi huo wakidai ilikuwa opresheni iliyofanywea kwa kushirikiana na wanapiganaji wa kundi la Al Aqsa linalohusiana na chama cha Fatah.