GAZA:Hamas kulipiza kisasi dhidi ya Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Hamas kulipiza kisasi dhidi ya Israel

Kundi la Hamas linalotawala huko Palestina limewatolea mwito waarabu pamoja na waislamu kuwashambulia wamarekani kwenye eneo la mashariki ya kati kulipiza kisasi shambulio la Israel dhidi ya wapalestina kaskazini mwa Gaza.

Tangazo hilo limetolewa na Khaled Mashal kiongozi wa tawi la hamas la al-Qassam baada ya wapalestina kiasi cha 18 kuuwawa na wengine 40 kujeruhiwa kwenye mashambulio ya makombora katika mji wa Beit Hanoun.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi la Hamas kutoa wito kama huo dhidi ya Marekani.

Utawala wa Israel umezungumzia masikitiko yake na kuanzisha uchunguzi juu ya mashambulio hayo ambayo yalilengwa kuwazuia wanamgambo kuvurumisha roketi ndani ya Israel.

Lakini imesema operesheni hiyo itaendelea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com