Gaza. Watoto wawili wa Kipalestina wauwawa na jeshi la Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Watoto wawili wa Kipalestina wauwawa na jeshi la Israel.

Majeshi ya Israel yamewapiga risasi na kuwauwa vijana wawili wa Kipalestina karibu na mpaka wa Israel na Gaza.

Shambulio hilo lilitokea karibu na makaazi ya zamani ya walowezi wa Kiyahudi.

Duru za Wapalestina zimesema kuwa vijana hao walikuwa sehemu ya kundi la watoto ambao wamekwenda katika eneo hilo kuogelea.

Jeshi la Israel limedhibitisha kuwa wanajeshi wamewapiga risasi Wapalestina kadha ambao walionekana wakitambaa kuelekea ukuta wa mkapa karibu na mji wa Beit Lahiya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com