1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Wapiganaji wawili wauwawa.

Katika eneo la ukanda wa Gaza , wapiganaji wawili wa Kipalestina wameuwawa wakati wa shambulio la anga la jeshi la Israel.

Wapiganaji wawili wengine wamejeruhiwa wakati ndege ya kijeshi ya Israel ilipofyatua kombora dhidi ya gari katika kitongoji cha Zeitun katika mji wa Gaza.

Wapiganaji wote hao wanne wametambuliwa kuwa wanachama wa kikosi cha mashahidi wa Al Aqsa, ambacho ni tawi la kijeshi la chama cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas cha Fatah.

Hii inakuja wakati magari kadha ya deraya ya jeshi la Israel pamoja na mabuldoza, yakisaidiwa na ndege za kivita , kuingia tena katika eneo la ukanda wa Gaza, yakiingia kiasi cha kilometa mbili ndani ya mji wa kaskazini wa Beit Hanun.

Tangu jeshi la Israel kuanza kuongeza operesheni zake siku ya Alhamis, Wapalestina 22 wameuwawa katika ukanda wa Gaza kwa mujibu wa duru za Kipalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com