Gaza. Wapalestina wapambana wao kwa wao. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Wapalestina wapambana wao kwa wao.

Majeshi ya usalama ya Palestina yanayomuunga mkono rais Mahmoud Abbas yamepambana na polisi wa Hamas mjini Gaza. Mapigano hayo ya silaha yalitokea katika eneo la kusini mwa ukanda wa Gaza katika mji wa Khan Younis.

Hali ya wasi wasi kati ya chama cha Abbas na chama cha Hamas imeongezeka tangu watu wenye silaha walipowapiga risasi watoto wa mkuu wa usalama na mfuasi wa chama cha Fatah wakati wakiwasili shule siku ya Jumatatu. Hakuna kundi lililodai kufanya mauaji hayo. Fatah na Hamas vimeshutumu shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com