GAZA. Wapalestina sita wauawa Ukanda wa Gaza
22 Aprili 2007Matangazo
Wapalestina sita wameuawa kufuatia mashambulio yaliyofanywa na ndege za Israel kwenye ukanda wa Gaza.
Maafisa wa idara husika wamesema kuwa wanaharakati wa kundi la al-aqsa na wa kundia la Islamic Jihad waliuawa wakati gari lao liliposhambuliwa na wanajeshi wa Israel katika mji wa Jenin.
Isreal imethibitisha kuwa majeshi yake yamewaua wanaharakati hao.