1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA : Wanajeshi wa Israel waingia kusini mwa Gaza

22 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPt

Wanajeshi wa Israel wameingia katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza katika operesheni ndogo inayolenga kutafuta mahandaki. Jeshi la Israel halikutoa matamshi yoyote kuhusiana na uvamizi huo.

Maafisa wa usalama wa Palestina wamesema vikosi vya Israel vimekuwa vikifanya harakati zake katika eneo la mpakani na hakuna malumbano yoyote baina yao na Wapalestina.

Operesheni za mpakani za aina hiyo zimekuwa nadra tangu kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo mwezi Disemba mwaka jana. Lakini Israel imekuwa ikionya kwamba wanamgambo wa kipalestina wanaendelea kuchimba mahandaki ya chini ya ardhi kutoka Gaza kuvuka mipaka na kuitumia kuingizia silaha kutoka Misri zinazotumiwa kuishambulia Israel.

Mwezi Juni mwaka jana wanamgambo wa kipalestina walichimba handaki kutoka Gaza na kuingia Israel ambako waliwaua wanajeshi wawili na kumteka nyara mwingine wa tatu katika uvamizi wa kituo cha kijeshi cha mpakani.