GAZA: Wafuasi watatu wa chama cha Hamas wauwawa
5 Julai 2007Matangazo
Majeshi ya Israel yameingia kati kati ya Ukanda wa Gaza na kuwauwa wafuasi watatu wa chama cha Hamas.
Walioshuhudia tukio hilo na duru za hospitali zinasema kwamba Wapalestina hao waliuwawa katika kambi ya wakimbizi ya al Maghazi katika mji wa Gaza.
Jeshi la Israel hata hivyo bado halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na mauaji hayo.