Gaza. Mwanajeshi wa Hamas auwawa katika mapambano. | Habari za Ulimwengu | DW | 02.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Mwanajeshi wa Hamas auwawa katika mapambano.

Majeshi ya usalama ya chama cha Hamas yamepambana na watu wenye silaha kutoka katika kundi hasimu katika ukanda wa Gaza. Mwanajeshi mmoja wa jeshi la Hamas ameuwawa na wengine kadha katika pande zote wamejeruhiwa.

Ghasi hizo zilizuka wakati majeshi ya chama cha Hamas yalipojaribu kutekeleza sheria ya kupigwa marufuku kuwapo na silaha iliyowekwa katika eneo la Gaza baada ya kuchukua udhibiti mwezi uliopita.

Wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa mvutano huo ulianza baada ya wanamgambo wa kundi la Islamic Jihad kufyatua risasi hewani katika sherehe za harusi.

Wakati huo huo majeshi ya Israel yamewauwa Wapalestina wawili na kuwajeruhi wengine kadha wakati walipoingia katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Hamas kaskazini ya ukanda wa Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com