GAZA: Mashauriano yaendelea vyema kuhusu askrai wa Israil anayeshikiliwa mateka. | Habari za Ulimwengu | DW | 01.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Mashauriano yaendelea vyema kuhusu askrai wa Israil anayeshikiliwa mateka.

Msemaji wa Hamas amesema kuna dalili za matokeo mazuri katika mashauriano yanayoendelea kuhusu kuachiliwa huru mwanajeshi wa Israel anayeshikiliwa mateka na kundi la wanamgambo wa Palestina.

Msemaji huyo hakutoa taarifa zaidi lakini alisema mashauriano hayo yameendelea vyema na huenda askari huyo Gilad Shalit akaachiliwa karibuni baada ya Israil nayo kuwaachilia huru wafungwa wa Kipalestina.

Shalit alitekwa mjini Gaza mwezi Juni hali iliyosababisha Israil kuushambulia ukanda wa Gaza ambapo mamia ya wapalestina waliuawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com