GAZA: Jeshi la Israel lafanya uvamizi | Habari za Ulimwengu | DW | 27.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Jeshi la Israel lafanya uvamizi

Ndege za Israel zimefanya shambulio la angani katika mji wa Beit Hanun, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema leo.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema shambulio hilo lililenga kifaa kinachotumiwa na wanamgambo wa kipalestina kuvurumishia maroketi aina ya Qassam kutoka eneo hilo kuelekea Israel.

Walioshuhudia wanasema hakuna aliyejeruhiwa kwenye shambulio hilo lililofanywa siku moja baada ya jeshi la Israel kufanya shambulio kama hilo ambalo halikusababisha majeruhi.

Hapo awali kundi la wanamgambo la Islamic Jihad limesema limevurumisha roketi kutoka eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kuelekea Israel. Hakuna ripoti zozote za majeruhi zilizotolewa nchini Israel.

Israel imekuwa ikifanya mashambulio kadhaa katika Ukanda wa Gaza tangu kundi la Hamas lilipolidhibiti eneo hilo mnamo mwezi Juni mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com