1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Hamas waweka masharti kwa waandishi.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1M

Kundi lenye imani kali la Hamas , ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza limeweka sheria kali dhidi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine wa vyombo vya habari. Hatua hizo zimetangazwa kama sehemu ya mpango wa kuzuwia mikusanyiko ya hadhara , kufuatia maandamano makubwa yaliyofanywa na waungaji mkono chama cha Fatah. Wafanyakazi wa televisheni ya Ujerumani walikamatwa kwa muda jana. Maafisa wamesema kuwa waandishi wote wa habari na wapiga picha ambao hawana kadi maalum zilizotolewa na Hamas hawataruhusiwa kufanyakazi katika eneo la Gaza.